Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema walia na IGP Sirro

Chademapic Kutoshiriki Chadema walia na IGP Sirro

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kumwachia au kumpeleka mahakamani mwanachama wake, Twaha Mwaipaya.

Leo ni siku ya tatu tangu jeshi la Polisi limshikilie Mwaipaya ambaye ni Mwenezi wa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (Chadema) bila kumpa dhamana.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 3, 2022 na Msemaji wa waliokuwa wagombea ubunge wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Celestine Simba.

Amesema iwapo mwanachama huyo ametenda kosa apelekwe mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria, badala ya kumshikilia bila hatua zozote.

"Kama ametenda kosa la kimtandao alipaswa kutaarifiwa aende Kituo cha Polisi apate huduma za wanasheria aione familia yake," amesema.

Celestine amesisitiza kuwa vijana wa chama hicho wana haki ya kufanya siasa kama ambavyo vyama vingine.

Advertisement Ametaka kuwepo uhuru na usawa katika ufanyaji wa siasa, huku akionya mwendelezo wa vitengo hivyo utasababisha kukosekana kwa uvumilivu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live