Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Chadema wakininyima udhamani, nitachaguliwa chama kingine"-Silinde

39720 Silindepic "Chadema wakininyima udhamani, nitachaguliwa chama kingine"-Silinde

Wed, 6 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Momba, David Silinde, amesema amemwandikia Mwenyekiti na Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiudhulu nafasi ya Katibu wa Wabunge wa chama hicho na Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara.

Waziri huyo kivuli amejiuzulu baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Easter Bulaya, aliyeandika kwenye mtandao wake wa Twitter kumkata kujiudhulu nafasi hizo kutokana kuhudhuria kikao cha bunge kinyume na agizo la Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe aliyewataka kujitenga kwa siku 14.

Amesema anaingia bungeni kuwakilisha wananchi wake ambao wanaweza kumchagua kupitia chama kingine.

"Watu wafahamu, tuko hapa bungeni kwa udhamini wa vyama vyetu na kupigiwa kura na wananchi, ikitokea siku Chadema wakaninyima udhamini wa chama chao, wananchi wa Momba wanaweza kunichagua kwa chama kingine, na hata Chadema wanaweza kunipa udhamini lakini wananchi wasinichague" amesema Silinde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live