Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema wakichaguliwa sadaka zitaongezeka - Sugu

D683ed3e959d72d1af2e7cf59063410f Chadema wakichaguliwa sadaka zitaongezeka - Sugu

Thu, 8 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ameomba viongozi wa dini wawaombe waumini wawachague wagombea kutoka chama hicho ili wananchi waweze kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada.

Sugu aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni kwenye kata ya Maendeleo. Alisema maisha ni magumu na sadaka zimepungua makanisani kwa kuwa waumini hawana fedha hivyo kusababisha viongozi wa dini nao kuishi maisha magumu.

“Viongozi wa dini niwaombe sana… Sio tu mtuombee kwa Mungu ili tushinde Oktoba 28...bali pia mtuombee kura kwa waumini wenu kwa sababu serikali ya Chadema ina sera nzuri za uchumi zinazokwenda kurudisha kipato kwenye mifuko ya waumini wenu ili sadaka ziongezeke…ili fungu la kumi liongezeke… ili zaka ziongezeke na kazi ya Mungu iendelee...kwa sababu sisi Mbeya ni wacha Mungu ndugu zangu,” alisema Mbilinyi.

Aliomba wananchi waliojiandikisha kupiga kura wasikubali kurubuniwa na watu wanaopita majumbani kuulizia vitambulisho

Chanzo: habarileo.co.tz