Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema wakanusha kuwepo mgogoro ndani ya chama

22433 CHADEMA+PIC TanzaniaWeb

Tue, 16 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam, Chadema kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Vincent Mashinji wametofautiana kwenye kikao cha Kamati Kuu.

Taarifa hizo zimesema kwamba viongozi hao wamekutana kwenye kikao kilichofanyika nyumbani kwa mwenyekiti mwishoni mwa juma hili. 

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema leo Oktoba 15, 2018 kwamba hakuna kikao chochote cha Kamati Kuu ambacho kimefanyika mwishoni mwa wiki hii, si tu nyumbani kwa mwenyekiti Mbowe bali popote pale.   

‘’Tunaomba Watanzania na wanachama wetu wapuuze taarifa hiyo potofu inayosambazwa kwenye mitandao,’’amesema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.

Amesema pia haijawahi kutokea wakati wowote vikao vya kamati kuu vikafanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz