Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema wajifungia Dar, kujadili mambo manne

49563 Pic+chadema

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Kamati Kuu ya Chadema imekutana katika kikao maalumu kujadili na kutoa mwelekeo wa masuala yanayojitokeza katika hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kikao hicho cha siku moja kitajadili maandalizi kuelekea Vikao vya Bunge la Bajeti litakaloanza siku chache zijazo, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Ajenda nyingine za kikao hicho chini ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kitajadili hatma ya ubunge wa Joshua Nassari na hali ya demokrasia nchini.

Akizungumza leo Machi 30, 2019 msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene amesema kikao hicho kitaibuka na ajenda za kitaifa baada ya kumalizika hapo baadaye.

"Katika kipindi hiki kuna matukio mengi yamejitokeza na mengine yatakayojitokeza kwa hiyo kikao kitajadili na kuangalia ushiriki wake katika mwelekeo wa Taifa ili kugusa mahitaji ya Watanzania, baada hapo kuna ajenda zitatokana na kikao hiki, tutawajulisha kwa taarifa nyingine zitakazotokana na kikao hiki hapo baadaye," amesema Makene.

Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya 2006, toleo la 2016, ibara ya 7:7:15 inayotoa maelekezo kwa kamati hiyo kukutana kwa ajili ya kujadili na kutoa mwelekeo wa masuala yanayojitokeza katika hali ya kisiasa nchini.

Katika ratiba ya vikao hivyo, kwa mara ya kwanza mwenyekiti huyo anakutana na wajumbe wa kamati hiyo tangu alipotoka rumande.

"Kikao kinaendelea na mwenyekiti amewashukuru wajumbe kwa umoja waliouonyesha akiwa rumande, pia amewashukuru wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa kuungana pamoja katika kudai demokrasia nchini," amesema Makene.



Chanzo: mwananchi.co.tz