Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema wafurahia kampeni za kutumia magari

9c58ab26c9f0bad5115445c96285ae80 Chadema wafurahia kampeni za kutumia magari

Fri, 2 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hatua ya kuzuiwa kutumia helikopta kwenye kampeni, kumekiwezesha kufanya mikutano mingi zaidi na kusababisha wananchi kufurika kusikiliza sera zao. Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Arusha na Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho, Tundu Lissu.

Alisema kuzuiwa huko na serikali, kwa kigezo kuwa rubani wao ana umri zaidi ya miaka 55 kumewezesha Chadema kutumia magari na kufanya mikutano kwa haraka zaidi, tofauti kama wangetumia helikopta.

Alisema watu wanajitokeza kusikiliza sera mbalimbali, kwani watanzania wanahitaji uhuru, haki na maendeleo yenye maisha ya maana.

Alisema wamekwenda mwambao wa Ziwa Tangayika na Ziwa Victoria, wananchi wanalalamika kuchomewa nyavu zao kutokana na uvuvi haramu .

Akizungumzia kuhusu Chadema kutosimamisha wagombea ubunge na udiwani katika baadhi ya mikoa, alisisitiza kuwa bado wanaendelea kufuatilia rufaa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).

Alisema hadi sasa wameshafikisha mwezi mmoja wa kufanya kampeni, sasa endapo NEC itawarejeshea rufaa wagombea udiwani au ubunge, baadhi ya wagombea watakosa haki zao za msingi za kusikilizwa.

Akizungumzia kukubali ushirikiano wa vyama vingine vya upinzani, alisisitiza kuwa wanaungana mkono katika maeneo ambayo Chadema hawana maslahi nayo na wametangaza hadharani kumuunga mkono Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad

Chanzo: habarileo.co.tz