Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema waanza maandamano Tanga

Chadema 598 Chadema waanza maandamano Tanga

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema muda huu Jumatatu Aprili 29, 2024 kimeanza maandamano yake mkoani Tanga.

Maandamano hayo yameanzia eneo la Duga Miembeni ambapo yanatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ambaye mpaka sasa hajaonekana miongoni mwa viongozi waliopo.

Viongozi waliopo, wakiwemo wa kitaifa hadi sasa, ni Naibu Katibu Mkuu – Bara, Benson Kigaila, Yosefa Komba Makamu Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini, Susan Lyimo, Spika wa Bunge la Wananchi na Amani Golugwa, katibu wa Chadema Kanda ya Kasikazini.

Askari Polisi wameonekana kujipanga barabarani kuyalinda maandamano hayo huku usafiri maarufu wa baiskeli jijijini Tanga ukiyaongoza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live