Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema waandaa ratibaya mikutano ya hadhara

42060 Mashinji+pic Chadema waandaa ratibaya mikutano ya hadhara

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema chama hicho sasa kinafanya uratibu na kupanga ratiba kwa ajili ya kuanza mikutano ya hadhara kama walivyoazimia katika azimio la Zanzibar.

Dk Mashinji amesema hayo leo Februari 15 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama chao kilichokaa Februari 9 na 10 katika Hoteli ya Bahari Beach.

"Tulikuwa na shughuli za kuimarisha chama na mambo mengine ya ndani ndiyo maana hatukufanya mikutano lakini sasa tunafanya maandalizi. Mikutano ni haki ya kikatiba hata aliyeizuia alifanya utashi wake binafsi si kwa msukumo wa kisheria," amesema Dk Mashinji.

Anasema vyama vya siasa vilijikuta vikitii amri isiyo halali kisheria na Serikali ilijificha katika kichaka kuwa wapinzani wanatumia mikutano hiyo kuwatukana na kuwakashifu wakati hawafanyi hivyo kwa kuwa chama kina sera ambazo kinataka kuzieleza kwa wananchi.

Ameongeza kuwa viongozi wa CCM sasa wanafanya mikutano ambayo Serikali yao iliizuia lakini mikutano yenyewe imejikita katika kejeli na kukashifu watu.

Kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, Dk Mashinji amesema wamejiandaa kwa ukubwa kwa kuwa hakuna uchaguzi mdogo na sasa wanafanya mapitio ya kanuni zote za uchaguzi huo.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz