Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema kuzindua mikutano Januari 21

Chademapic 600x400 Chadema kuzindua mikutano Januari 21

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: Mwananchi

Siku tatu baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza ruhusa ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuzindua rasmi mikutano hiyo.

Rais Samia alitangaza uamuzi huo, Januari 3, 2023 alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa na alisema: “Uwepo wangu mbele yenu ni kuja kutoa ruhusa kwamba lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa”.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 6, 2023 na chama hicho na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema imesema maazimio hayo yanatokana na Kamati kuu iliyoketi Januari 5, mwaka huu

“Kamati Kuu katika kikao chake cha dharura Januari 5, 2023 ilipokea na kujadili mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano baina ya timu ya Chadema inayoongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Abdulrahman Kinana,” imeeleza taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa ya Chadema, Januari 21, 2023 itazindua rasmi mikutano ya hadhara kitaifa, itakayofuatiwa na uzinduzi wa mikutano ya hadhara katika kila Makao Makuu ya Kanda na baadaye ngazi nyingine za chama hicho.

Hata hivyo, ngazi zote za chama hicho zimeagizwa kuendelea na maandalizi ya mikutano ya hadhara. Kamati Kuu ya Chadema imeazimia kuendelea kwa mazungumzo ya maridhiano kati yake na CCM yanayoendelea kwa kile ilichokieleza kuwa imeridhishwa nayo.

Chanzo: Mwananchi