Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema kutekeleza ahadi za marehemu Bilago

11692 Chademaaaa+pic TanzaniaWeb

Wed, 18 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Wakati kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Buyungu zikiendelea, Chadema mkoa wa Kigoma kimeahidi kutekeleza miradi yote ya maendeleo katika jimbo hilo iliyoanzishwa na aliyekuwa mbunge wake, marehemu Kasuku Bilago.

Bilago alifariki Mei 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ambapo marudio ya uchaguzi huo utafranyika Agosti 12, 2018.

Katibu wa Chadema mkoa wa Kigoma, Shabani Madede akizungumza na Mwananchin leo Julai 18, 2018 amesema ahadi zilizotolewa mwaka 2015 kwenye kampeni za uchaguzi bado wanazitambua.

Amesema chama hicho kimemsimamisha Diwani wa Gwarama, Elia Kanjero kugombea ubunge katika uchaguzi huo na imani yao miradi itakayopewa kipaumbele ni ya ujenzi wa barabara, maji, vituo vya afya na zahanati, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo vya shule.

Madele amesema licha ya kampeni za uchaguzi kuzinduliwa Julai 15, 2018 Chadema wanatarajia kuanza mikutano yao Julai 22, ambapo mkutano wa kwanza utafanyika Kakonko mjini au kata ya Kasanda.

Kanjero katika uchaguzi huo, atachuana na mgombea wa CCM, Mhandisi Christopher Chiza ambaye tayari amekwisha kuanza kampeni.

Soma Zaidi:

Bilago azikwa kijijini Kasuga

Utata waibuka mazishi ya Bilago

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz