Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema kueleza ‘hujuma’ uchaguzi kata ya Turwa

11714 Pic+chadema TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitisha mkutano wa waandishi wa habari leo mchana Jumatatu Agosti 12, 2018 mjini Tarime kuzungumzia kile wanachodai kuwa ni hujuma zilizofanyanywa dhidi ya mgombea wao kata ya Turwa.

Akizungumza na MCL Digital katibu wa Chadema mkoa wa Mara, Chacha Heche amesema chama hicho kinatarajia kutumia nakala za fomu za matokeo ya vituoni kutoa ushahidi kuthibitisha hujuma hizo.

Amesema waliotekeleza hujuma hizo ni watendaji na wasimamzi wa uchaguzi huo uliofanyika jana Agosti 12, 2018 na mgombea wa CCM, Chacha Ghati kutangazwa mshindi.

Katika uchaguzi huo, Chadema ilimsimamisha Charles Mnanka aliyepata kura 1,121 dhidi ya kura 1,401 alizopata Ghati.

Chanzo: mwananchi.co.tz