Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema chasisitiza kutosusia uchaguzi mkuu

22586 CHADEMA+PIC Chadema chasisitiza kutosusia uchaguzi mkuu

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kuwa katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba 25, mwaka huu kitashiriki kwa asilimia mia katika nafasi zote, licha ya kuwapo kwa mazingira ya kufanyiwa figisu.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kutoka Bara, Benson Kigaila, aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa watiania wa nafasi ya ubunge kutoka Kanda ya Serengeti, inayounda mikoa ya Simiyu, Mara, pamoja na Shinyanga.

Alisema chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana, kilijitoa kushiriki kwenye uchaguzi huo baada ya kuona kuwapo na mazingira ya kufanyiwa rafu na kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu mazingira ni hayohayo, na kusisitiza kuwa hakitajitoa bali kitapambana.

“Niwaambie tu watia nia wa nafasi ya ubunge na udiwani wa chadema, uchaguzi mkuu wa mwaka huu hakuna wa kujitoa, tuna jua kuna mazingira yameandaliwa ya kufanyiwa rafu, ambapo hakuna tume huru, katiba, na utungwaji wa sheria za kutubana, lakini tutapambana hivyo hivyo na tutashindia kituoni watake wasitake.” alisema Kigaila na kuongeza:

“Tunachotakiwa ndugu zangu ni kwenda kupitisha wagombea ambao wanakubalika na wananchi na wenye moyo wa kuwatumikia katika kutatua matatizo yao, na watakaojenga hoja majukwaani, sababu tunajua wenzetu hawana hoja zaidi ya kujipanga kutumia dola na tukifanya hivyo tunawashinda kweupe,” alisema Kigaila.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, Ester Matiko, ambaye alikuwa mbunge wa Taarime mjini, nae ametia nia kutetea jimbo hilo, aliwatoa hofu watiania wenzake kwa kuwaeleza kuwa hakuna mgombea ambaye atashinda na asitangazwe.

Matiko aliwataka watiania wote kuungana na kuwa kitu kimoja na kumkubali yule ambaye atashinda kwenye kura za maoni ndani ya chama, na kupitishwa kuwa mgombea wa Jimbo au Kata na siyo kuunda makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live