Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema Wafungua Kesi Kudai Dhamana

Hashim Issa Juma Chadema Wafungua Kesi Kudai Dhamana

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua kesi kudai kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa Baraza la Wazee la chama hicho, Hashim Issa Juma (63) ambaye anashilikiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa siku ya nne sasa.

Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari CHADEMA wanasema licha ya kufanya utaratibu wote kumuombea dhamana kiongozi huyo bado polisi wameendelea kumshikilia.

Kufuatia hayo, timu ya wanasheria wa chama hicho wamefungua shauri mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam, wakitaka jeshi la polisi kueleza kwa nini hawataki kumpatia dhamana mtuhumiwa huyo wakati ni haki yake ya kikatiba.

Akizungumzia sakata hilo Jumanne, Kamanda wa kanda maalumu ya jeshi la polisi Dar es salaam Jumanne. Muliro alisema jeshi hilo bado linamshikilia mwenyekiti wa baraza la wazee wa CHADEMA Hashimu Issa Juma kwa tuhuma za kutoa kauli za kichochezi.

Kamanda Muliro anasema wanamhoji kwa kina baada ya tarehe 01/10/2021 akiwa eneo la ufipa kinondoni kutoa kauli za kichochezi zilizokuwa na nia ya kujenga chuki kati wananchi na serikali. Hashim alikamatiwa visiwani Zanzibar na baadae kurejeshwa Dar es salaam ambako alitolea kauli zinazodawa kuwa ni za kichochezi.

Jeshi la polisi linaendela kukusanya ushahidi ili kuhakikisha hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa sheria‘’. Jeshi la polisi linakusanya ushahidi wote kwa kadiri inavyowezekana na litahakikisha hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa huyu zinafanyika kwa kufuata mtiririko wa kisheria’’ Alisema Kamanda Muliro.

Chanzo: globalpublishers.co.tz