Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema: Hatuko tayari kuziachia fedha za ruzuku

CHADEMAPIC 660x400 Chadema: Hatuko tayari kuziachia fedha za ruzuku

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kiko tayari kuchukua fedha za ruzuku kutoka Serikalini, kutokana na maridhiano yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akihojiwa na Kituo cha redio cha Wasafi FM, leo tarehe 19 Januari 2023, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Chadema, Rodrick Lutembeka, amesema watakuwa wajinga kama hawatapokeo kitu kinachotokana na maridhiano yanayofanyika kati ya Serikali na vyama vya siasa vya upinzani.

“Ikitokea kwa mazingira ya sasa hivi, sababu hata wakati ule wangeweza kuidumbukiza (akaunti ya benki) tusingeweza ichukua lakini kwa mazingira ya sasa hivi wakati tunaendelea na mazungumzo ya maridhiano Chadema tutakuwa wajinga sana kutoweza kupokea kile ambacho kinatokana na maridhiano.” alisema Lutembeka lipoulizwa kama Chadema kiko tayari kuchukua ruzuku.

Mkurugenzi huyo wa fedha Chadema, amesema malimbikizo ya fedha za ruzuku ambayo chama hicho kimegoma kupokea kutoka Serikalini tangu 2020, yamefikia zaidi ya Sh. 2 bilioni.

Amesema kuwa, Chadema kimekuwa kikijiendesha kupitia michango ya wanachama wake.

Akizungumzia kuhusu maridhiano yanayofanywa na Serikali pamoja na vyama vya siasa vya upinzani, Lutembeka ameeleza kuwa, matokeo yake yameanza kuonekana, ikiwemo kuondolewa zuio batili la mikutano ya hadhara, urekebishwaji wa sheria kandamizi ikiwemo sheria za uchaguzi, na ufufuaji mchakato wa upatikanaji katiba mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live