Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema: Aliyepitishwa kuwania uenyekiti mtaa wa muungano sio mgombea wetu

82615 Chadema+pic Chadema: Aliyepitishwa kuwania uenyekiti mtaa wa muungano sio mgombea wetu

Sat, 2 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema mgombea wake wa uwenyekiti mtaa wa Muungano kata ya Goba jijini Dar es Salaam, Said Mponda amekataliwa kupewa fomu kwa maelezo kuwa zimechukuliwa na mgombea mwingine wa chama hicho, Peter Urio.

Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene baada ya viongozi wa Chadema kuhoji  barua ya udhamini iliyotolewa na Urio hadi kukubaliwa kupatiwa fomu, msimamizi msaidizi, Lightness Shirima aligoma kuwaonyesha.

Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu suala hilo, Lightness alikataa kuzungumzia suala hilo na kutaka zitafutwe mamlaka za juu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Novemba Mosi, 2019 katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Kibamba, Nelson Muhanga amesema wamepeleka barua kwa ajili ya kutengua uteuzi wa mgombea huyo ambaye hawamtambui lakini msimamizi huyo alikataa kuitambua.

“Tulipeleka barua ya katibu wa Chadema kata kutengua uteuzi huo lakini msimamizi akakataa. Tukapeleka tena barua ya katibu wa jimbo akakataa. Kesho tunapeleka tena barua ya katibu wa wilaya, akikataa na hiyo tunakwenda mahakamani,” amesema Muhanga.

Amesema jambo hilo si sawa na madai kuwa mgombea wa CCM uteuzi wake ulitenguliwa Jumanne Oktoba 29, 2019 na chama hicho kuteua mgombea mwingine ambaye alipatiwa fomu, kuhoji sababu za wao kukataliwa. Muhanga amesema kuna hila zinazofanywa na wasimamizi wa uchaguzi kubainisha kuwa wataendelea kupigania haki za wananchi kupata viongozi wanaowataka kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao.

“Haya mambo yana utaratibu wake nimeshasema mimi siwezi kuongea. Mtafute msimamizi wa uchaguzi ndiyo azungumze,” alisema Shirima.

Chanzo: mwananchi.co.tz