Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema, ACT wafanya mazungumzo ya ushirikiano

11399 Chadema+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa ubunge jimbo la Buyungu na Kata 79, vyama vya Chadema na ACT-Wazalendo vimeanza mazungumzo ya kushirikiana  katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12, 2018.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Julai 13, 2018 jijini Dar es Salaam, huku ACT ikiwakilishwa na Omar Said Shaaban ambaye pia ni rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS).

Timu ya Chadema katika mazungumzo hayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Oganaizesheni  na Uchaguzi,

Akizungumza na MCL Digital, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema baada ya kumalizika kwa mazungumzo wamewaachia jukumu Chadema kwenda kujadiliana.

“Tulichokizungumza wenzetu wa Chadema  wanayajadili katika ngazi ya sekretarieti kabla ya kufanya makubaliano ya mwisho. Hekima inatutaka kuwasubiri wenzetu wajadiliane, waafikiane na kisha tufanye makubaliano ya mwisho. Tunasubiri,” amesema Shaibu

Chanzo: mwananchi.co.tz