Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chacha Heche ashinda usenyekiti Chadema Mara akiwa nje ya nchi

Chacha Heche Ashinda Usenyekiti Chadema Mara Akiwa Nje Ya Nchi Chacha Heche ashinda usenyekiti Chadema Mara akiwa nje ya nchi

Thu, 28 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara, Chacha Heche amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho akiwashinda wagombea wenzake wawili.

Heche ambaye yupo nchini India alikomsindikiza ndugu yake kwenye matibabu, ameomba kura kwa njia ya mtandao, kwenye uchaguzi uliofanyika mjini Musoma jana Machi 27, 2024.

Akitangaza matokeo hayo, mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo, Suzan Kiwanga amesema Heche amepata kura 59 sawa na asilimia 53; huku wenzake Bashiri Selemani na Jacob Maiga wakipata kura 25 kila mmoja kwenye awamu ya pili ya upigaji kura.

Uchaguzi huo ulirudiwa mara ya pili baada ya awamu ya kwanza wagombea wote kutokufikisha nusu ya kura kwa mujibu wa kanuni. Awali Heche alipata kura 52 huku wagombea wenzake kila mmoja akipata kura 29. “Kwa nafasi ya uenyekiti wa mkoa, namtangaza ndugu Chacha Heche aliyepata kura 59, sawa na asilimia 53 dhidi ya Selemani aliyepata asilimia 22.7 na Maiga ambaye pia amepata asilimia 22.7,” amesema Kiwanga.

Katika uchaguzi huo ambao ulimalizika usiku wa manani, Donald Mwembe alichaguliwa kuwa katibu baada ya kupata kura 60 dhidi ya Angela Lima aliyepata kura 45 na Deus Kaki aliyepata kura sita.

Akizungumza kwa njia ya mtandao baada ya kuchaguliwa, Heche amewashukuru wajumbe kwa kumwamini na kumpigia kura licha ya kuwa hakuwepo ukumbini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live