Dar es Salaam. Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe amejiuzulu uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania na kujiunga na CCM leo Jumamosi Februari 15, 2020.
Mwambe ambaye takribani miezi miwili iliyopita alijitosa kugombea uenyekiti wa Chadema akichuana na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ametangaza uamuzi huo mbele ya katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole. Katika uchaguzi huo Mwambe alishindwa na Mbowe.
Akizungumza kuhusu uamuzi wake huo Mwambe amesema vyama vya upinzani nchini vina safari ndefu ya kujenga demokrasia ya kweli, ameona atakuwa anajidanganya na kuwadanganya wapiga kura wake kubaki katika vyama vya namna hiyo wakati bado anatamani kuwatumikia wananchi wa Ndanda.
“Leo kwa kuamua mwenyewe nimeamua kujiunga na CCM kama mtanipokea na kunikaribisha basi nipewe tena nafasi ya kugombea endapo mtaridhia na nitapata nafasi,” amesema Mwambe.
SOMA ZAIDI
Pia Soma
- Masharti mapya vitambulisho vya machinga
- Wahamiaji haramu tisa wa Kenya wakamatwa Dodoma Tanzania
- Matumizi ya karatasi utoaji dawa vituo vya afya marufuku
Paia amesema uamuzi wake wa kugombea uenyekiti na Mbowe uliibua chuki na laianza kuandamwa.
Naye polepole amesema Mwambe ametumia haki yake ya kikatiba na hivi karibuni waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye alifanya hivyo kwa kurejea CCM.
Polepole amemhakikisha Mwambe kwamba katika chama anachojiunga uwazi wa mapato na matumizi upo wa kiwango cha juu na kila kitu kipo kielektroniki na kwa zaidi ya miaka miwili kimepata hati safi.
“Karibu sana nitawafahamisha viongozi wakuu wa juu wa chama kuu nia yako njema,” amesema Polepole.
Alichokisema Magufuli kuhusu Mwambe
Oktoba 15, 2019 Rais wa Tanzania, John Magufuli alisema 'figisu' ndani ya CCM zilisababisha Mwambe kugombea ubunge wa Ndanda kwa tiketi ya Chadema.
Alieleza hayo aliposimama njiani kuzungumza na wakazi wa Ndanda wakati akielekea Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
“Mbunge wenu huyu (Mwambe) alikuwa mgombea wa CCM (mwaka 2015) anakubalika lakini kwa sababu ya figisu za watu wa huku (CCM) nataka nieleze ukweli mimi huwa napasuaga tu wakaacha kumpitisha akaamua kuhama CCM."
"Kwa hiyo huyu ni wetu mlifanya makosa wenyewe na mnafahamu makosa ya kukosea kuchagua,” amesema Magufuli.
Amesema Mwambe alitakiwa awe mbunge wa CCM, alimuita mbunge huyo azungumze kuhusu suala hilo.
SOMA ZAIDI
- VIDEO: Mbunge wa Ndanda atangaza kugombea uenyekiti Chadema
VIDEO: Rais Magufuli asema CCM walichangia mbunge Mwambe kuhamia Chadema
“Lakini Mungu alichagua niwe kiongozi wa Ndanda, nilikwenda Chadema nikashinda, nina ahidi nitaendelea kushirikiana na wananchi wa hapa."
Baada ya Mwambe kueleza hayo Rais Magufuli amesema, "wakati mwingine tunajicheleweshea maendeleo sisi wenyewe. Mtu anapendwa na wananchi, anakipenda chama lakini figisu za chama mnamnyima mtu anayetaka kushiriki. Hili liwe fundisho kwa wanachama na wananchi wa huku.”
“Mimi niligombea (waliojitokeza kupitishwa kuwania urais CCM mwaka 2015) na watu 42 wa CCM ila kiukweli mimi nilikuwa nakubalika hawakunifanyia mzaha wakanipitisha. Wanaokubalika msiwafanyie figisu hiki ni chama chetu wote.”
Ameongeza, "nimekusikia hata ninapokuona moyo wako umejaa CCM ninakuamini na kama upo tayari kuhamia CCM uhamie, msimkate tena ninahitaji watu watakaonipa ushauri mzuri kwa kuwa tunaongea lugha moja inayofanana kama ilivyo kwa Nape (Nnauye-mbunge wa Mtama- CCM)."