Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF yawaonya wabunge wake

48786 Wabungepic

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wabunge wa CUF waliokuwa wanamuunga mkono aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad wametakiwa kujitafakari la sivyo hawatavumiliwa.

Machi 18, 2019 Maalim Seif alijiunga na chama cha ACT-Wazalendo sambamba na mamia ya wanachama wakiwemo waliokuwa viongozi wakuu wa chama hicho.

Ujumbe kwa wabunge hao umetolewa leo Jumanne Machi 26, 2019 jijini Dodoma na makamu mwenyekiti wa CUF, Maftah Nachuma wakati akizungumza na waandishi wa habari, kusisitiza kuwa mgogoro wa chama hicho umekwisha.

Nachuma ambaye ni mbunge wa Mtwara Mjini amesema wabunge wote wanatakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja ili kukiimarisha chama hicho baada ya misukosuko mingi.

“Chama hakiwezi kumvumilia mtu ambaye atakuwa mbunge kupitia chama chetu lakini akaonekana anatumia vibaya rasilimali yetu kwa kuunga ama kushabikia chama kingine, bora ajitoe mapema kabla ya kushughulikiwa," amesema Nachuma.

Huku akisifu utendaji kati wa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Nachuma amesema waliohama chama hicho wanatakiwa kuwa wastaarabu na kuacha kuharibu mali za chama chao.



Chanzo: mwananchi.co.tz