Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF yatamba kuibuka washindi wa urais Z’bar 2020

52149 Pic+ushindi

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kitashinda uchaguzi mkuu wa 2020 kwa nafasi ya urais visiwani Zanzibar.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Aprili 13, 2019 na Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Sulemain wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi katika mkutano wa ndani uliofanyika Amani mjini Unguja.

Amesema kwa sababu wana mikakati imara na kukubalika na umma hana shaka ya ushindi huo na wanajipanga kuweka mazingira sawa zaidi.

Katika hatua nyingine amesema wakati umefika wa kupingana na matendo hya udhalilishaji na wananchi wasikubali tena kudhalilishwa na wawafikishe kwenye vyombo vya sheria wahusika.

Hata hivyo, Khalifa amesema kwa sasa mikakati zaidi inaandaliwa kukijenga upya chama hicho ikiwemo kurudi kuwa wamiliki wa matawi yote ya chama hicho.

Khalifa amesema siasa isiwe sehemu ya chuki na kila mtu yupo huru kufanya siasa katika chama anachokitaka.

Akizungumzia kuhusu baadhi ya wanachama na viongozi kuhama chama hicho amesema hawajatetereka na kwamba chama chao kitakua salama muda wote.

“Watuachie chama chetu kama wafuasi na sisi tunao na sisi si majambazi kama wao hivyo tufanye siasa kwa amani na utulivu,” amesema.

Katibu mkuu huyo amesema anafahamu kwa kina wanayoratibu baadhi ya watu ambao hakuwataja majina kuwa wana mkakati maalumu wa kuingiza nchi kwenye machafuko ili wapate mwanya zaidi na maslahi yao.

Naye makamu mwenyekiti wa chama hicho- Zanzibar, Abbas Juma Muhunzi amesema CUF kiliingia kwenye mgogoro baada ya aliyekuwa katibu mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad kutofahamu dhamira ya Profesa Lupumba kufuatia kujiuzulu kwake.

Amesema kwa sababu Maalim Seif alishindwa kufahamu dhamira ya Profesa Lipumba ambayo ilikua ni kulinda heshima yake ikapelekea chama hicho kuwa na mpasuko mkubwa ambapo matokeo yake chama hicho kimegawanyika.

Muhunzi amesema wakati umefika kwa viongozi wa sasa na wanachama kukataa kubaguliwa na kutenganishwa, kilichobaki wafanye kazi kwa umoja wao.



Chanzo: mwananchi.co.tz