Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF yapitisha 12 kugombea ubunge EALA

Cufpic Data CUF yapitisha 12 kugombea ubunge EALA

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Chama cha Wananchi (CUF) kimepitisha majina 12 ya wagombea wa nafasi ya Ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Akizungumza leo Agosti 22, 2022 Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema wagombea hao waliopitishwa watagombea kwenye makundi manne.

Ameyataja makundi hayo kuwa ni ya wanawake, wawakilishi kutoka Zanzibar, vyama vya upinzani na kundi la wagombea kutoka Tanzania bara.

Majina yaliyopitishwa na baraza hilo ni Adui Seif Kondo, Mashaka Ngole, Mneke Said, Muhamed Ngulangwa, Queen Lugembe, Sonia Magogo, Thomas Malima, Zainab Abdul na Zainab Amir wote kutoka Tanzania Bara,

Wengine ni Mohamed Habib Mnyaa,Husna Mohamed Abdallah na Anderson Emmanuel Ndambo wote kutoka Zanzibar.

"Tulipata maelekezo kutoka kwa katibu wa bunge kuwa vyama vyenye wawakilishi bungeni wanaweza kuteua watu watakaowawakilisha kwenye EALA katika makundi hayo manne, ndio maana tukateua wagombea 12 ambao kwenye nafasi moja wanaweza kugombea wakiwa watatu," amesema.

Katika hatua nyingine Profesa Lipumba ameitaka Serikali kusitisha tozo za miamala ya simu na miamala ya benki akiitaja kuwa ni kandamizi kwa wananchi.

Amesema tozo hizo zitachangia kudhoofisha mitaji ya wafanyabiashara na kuchochea wananchi kuanzisha utaratibu wa kuhifadhi fedha ndani.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz