Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF yajigamba kumbwaga Mtulia na Salum Mwalimu Kinondoni

1853 Bendera TZW

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkurugenzi wa Habari Uenezi (CUF),Abdul Kambaya amesema kuwa watashinda Jimbo la kinondoni kwasababu katika Jimbo hilo Chama hicho kipo kwa muda mrefu sana.



Akizungumza na Azam News, Kambaya amesema kuwa kiasili Jimbo hilo kiasili ni la watu maskini hivyo lazima washinde katika jimbo hilo.

“Baada ya Mtulia kuhama tutashinda kwasababu Kinondoni ni Jimbo kiasili ni jimbo la watu maskini sana ni chama cha CUF kipo muda mefu sana, chama cha CUF kina madiwani katika Kata 3 kati ya Kata 10 zilizopo pale wenzetu Chadema wana Kata mbili pale na hizo wamezipata kwa hayo hayo wanayoyaita maridhiano,“ alisema Kambaya.

“Mgombea tunae mnadi ni mzaliwa wa Kinondoni Jimbo la Kinondoni mkazi wa Kinondoni mpiga kura wa Kinondoni tangu tofauti na mgombea aliyeletwa na Chadema mpiga kura w kikwajuni lakini wapiga kura wa Kinondoni wanaweza kupima kama angelikuwa anahitaji maslahi ya Kinondoni tangu 2015 angegombea Kinondoni akawa mpiga kura wa Kinondoni kwa msalahi ya wana kinondoni maslahi ya Salum Mwalimu ni ya Kikwajuni na kwa upande wa Zanzibar jambo ambalo si baya kisheria anaruhusiwa kwahiyo utashi wake wa kwanza ni Kikwajuni wa pili labda ndio Kinondoni kwahiyo wanakinondoni sio spear tairi kwamba ikiharibika hii unapachika nyingine hapana wanamjua mgombea wao wanamjua mtu ambaye watampigia kura.“

Chanzo: bongo5.com