Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF wapinga kauli ya Mkurugenzi NEC

13262 Cuf+pic TanzaniaWeb

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Wananchi Cuf kimepinga kauli ya Mkurugenzi wa uchaguzi kuwa wagombea wa upinzani walitaka kurudisha fomu za kugombea ubunge katika ofisi zisizo sahihi.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa umma wa CUF, Abdul Kambaya amesema kauli hiyo ya mkurugenzi inatia aibu na kuichafua serikali kwa kuwa wapinzani walirudisha fomu katika ofisi waliyokabidhiwa.

Amesema si kweli kwamba mgombea wa CCM Korogwe alipita bila kupingwa bali alipitishwa kwa hujuma.

Amesema tangu saa sita mchana mgombea wa CUF na wengine wa vyama vya upinzani walifika katika ofisi hizo lakini hawakumkuta mkurugenzi.

"Kauli hii ni ya aibu, wanatoa majibu rahisi katika maswali magumu, kama serikali haitaki uchaguzi turudi kwenye mfumo wa chama kimoja,"

"Chaguzi hizi zinaichafua nchi, alichokifanya mkurugenzi wa Korogwe ni aibu na amedhihirisha ameshindwa kuisaidia CCM hadi akafikia hatua ya kuzuia wagombea wa vyama vingine wasishiriki,"

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi wa CUF Taifa, Masoud Omari amesema alikuwepo siku ya kurejesha fomu wakiwa pamoja na mgombea wa CCM.

"Kilichofanyika ni kitu cha ajabu yaani wagombea wote walikuwa pale hadi wa CCM akiwa na fomu yake lakini yeye akarudisha halafu siye tunaambiwa tumepotea ofisi,"

“Mgombea wa CCM ghafla akatoweka na kwenda kwenye kichumba kumbe huko ndiko alikopeleka fomu yake, baadaye tunaona mkurugenzi anatoka nje akiwa na ulinzi wa polisi akabandika fomu moja tu, wagombea wetu wakabaki na fomu zao mkononi,"amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz