Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF wamshukia Mtatiro, wadai ndiye chanzo cha migogoro

11471 MTATIRO+PIC TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku moja baada ya mwenyekiti wa baraza la uongozi chama cha CUF, Julius Mtatiro kutangaza kuhamia CCM, mkurugenzi wa habari, uenezi na uhusiano wa umma wa chama hicho,  Abdul Kambaya amesema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ndani ya chama hicho imechangiwa na Mtatiro.

Mtatiro aliyekuwa upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, jana Jumamosi Agosti 11, 2018 alitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga na CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Agosti 12, 2018, Kambaya ambaye yupo upande unaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mtatiro akiwa mwenyekiti wa mkutano mkuu alisababisha chama hicho kugawanyika kwa kutosikiliza maoni ya wajumbe wa mkutano huo na kuamua kuuendesha kibabe.

Amesema Mtatiro akiwa naibu katibu mkuu alikiingiza chama hicho katika mgogoro uliosababisha Hamad Rashid kufukuzwa uanachama baada ya kuhoji ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh300milioni katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga.

"Hakuna kitu ambacho Mtatiro amekifanya kwenye chama hiki, kubwa zaidi amesababisha migogoro. Wanasiasa wapambanaji hawakimbii  migogoro ndani ya vyama vyao bali wanakaa humo humo mpaka migogoro itakapokwisha” amedai Kambaya.

“Tazama Sophia Simba hakukimbia CCM sambamba na Nape Nnauye (mbunge wa Mtama-CCM). Hata Mnyika (John-Mbunge wa Kibamba-Chadema) hakukimbia chama hicho.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz