Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF wamnadi Salama jimbo la Ukonga

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu wa CUF Wilaya ya Ilala, Ally Maningi amesema Cuf ndiyo Chama peke chenye uwezo na dhamira katika kusimamia wananchi kwa misingi, taratibu na sheria.

Maningi ameyasema hayo leo (Jumamosi) Septemba 8 2018 wakati akimnadi mgombea wa chama hicho Salama Masoud katika mkutano wa kampeniĀ  zilizofanyika Chanika Mwisho.

Amesema dhamira hiyo ndiyo iliyowafanya wadai tume huru ya uchaguzi na kudai katiba mpya.

"Damira hiyo tulienda nayo mpaka tukagengeneza rasimu inayoelekeza nchi hii inaongozwa kwa sheria na taratibu,"amesema.

Amesema Salama ni mwanamke pia ni mwalimu hivyo atakuwa mlezi mzuri kwa watoto, vijana pamoja na kutatua matatizo ya wananchi.

"Kama mnataka suluhu ya matatizo yenu mchagueni Salama mgombea pekee wa chama kinachojali shida za watu,"amesema.

Kwa upande wake mgombea wa Jimbo la Ukonga (CUF)Salama amesema, endapo atatangazwa kuwa mbunge Septemba 16 jambo la kwanza atakalofanya ni kujenga kituo cha daladala.

"Nilivyokuja hapa nilitegemea nitafanya mkutano kwenye kituo cha daladala lakini imekuwa sivyo, kwa hiyo nitakwenda kutengeneza kituo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa chanika,"amesema.

Salama ameongeza kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hiloatahakikisha anaboresha mazingira ya biashara kwa wananchi wa Chanika.

"Pia nitashughulikia suala la afya, kwa sababu niuhimu kwa kila mwananchi, lakini pia sitawaacha nyuma vijana na wakina mama,"amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz