Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF walia rafu uchukuaji fomu uchaguzi Serikali za mitaa

82504 Cuf+pic CUF walia rafu uchukuaji fomu uchaguzi Serikali za mitaa

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa amedai baadhi ya watendaji wa Serikali ya Tanzania wanaingilia uchaguzi wa Serikali za mitaa, “hii inaweza kusababisha vurugu.”

Khalifa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 katika uzinduzi wa programu ya elimu ya mpiga kura iliyoandaliwa na mtandao wa Haki Yangu Mtanzania na kuwahusisha wanasiasa na waandishi wa habari.

Mbunge huyo wa zamani wa Gando kisiwani Pemba amesema licha ya miongozo ya baadhi ya vyama vya siasa kueleza mgombea katika uchaguzi huo atadhaminiwa na kiongozi wa ngazi ya chini,  baadhi ya watendaji wamekuwa wakidai udhamini wa viongozi wa juu.

“Muhuri wa chama tunaoutumia upo hadi kwa msajili na utatumika kuwa endorse (kuwaridhia) wagombea wetu. Anapokuja kiongozi yoyote akisema anataka muhuri wa katibu mkuu, anamaanisha nini,  kwani tumempa muhuri,” amehoji.

Amewaonya watendaji wa Serikali aliodai kuwa wanatafuta kuwafurahisha viongozi bila kujua kuwa wanavuruga uchaguzi.

 “Uchaguzi unakaribia hasa wa Serikali za Mitaa. Viongozi wanaosimamia uchaguzi wawe responsible (wawajibike),”  amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz