Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF wadhibiti ofisi zake za makao makuu Zanzibar

48756 OFISIPIC

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Chama cha wananchi CUF kimedhibiti ofisi zake kuu visiwani Zanzibar zilizopo Mtendeni mjini Unguja leo mchana Jumanne Machi 26, 2019.

Zoezi hilo limeongozwa na mjumbe wa bodi ya wadhamini, Mussa Haji Kombo pamoja na wanachama wengine wa chama hicho.

Wakati hayo yakijiri ulinzi mkali umeimarishwa katika eneo hilo huku bendera za chama hicho zikiwa zinapepea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kombo amesema wamelazimika kuweka bendera wakifahamu kuwa ofisi hiyo ni miongoni mwa mali za chama hicho.

Amesema wataendelea na utaratibu wa kuhakiki na kuzipitia ofisi zote za chama hicho Unguja na Pemba.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz