Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF hali si shwari

Cuf Pic Data CUF hali si shwari

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wajumbe wa kamati tendaji ya CUF Wilaya ya Kinondoni na ile iliyovunjwa kwa tamko la mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba wamegombania kutumia ofisi ya wilaya huku kila upande ukidai una haki ya kuitumia.

Katika Mvutano huo uliotokea leo Alhamisi Desemba 16,2021, kundi la wajumbe wa kamati iliyovunjwa na Lipumba Desemba Mosi, 2021 kwa madai ya makosa mbalimbali ikiwemo kushabikia viongozi ngazi ya Taifa kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii,  limesema  bado ni viongozi halali kwa sababu hawajapewa barua rasmi inayoonyesha nafasi walizoshika zimekoma.

Kundi la pili la wajumbe walioteuliwa juzi na Profesa Lipumba kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Kinondoni wanasema wao wana uhalali wa kutumia ofisi hiyo kwa kuwa wanatambulika na mwenyekiti wa chama hicho.

Hata hivyo, mkurugenzi wa habari, uenezi na mahusiano ya umma wa chama hicho, Mohamed Ngulangwa amesema wanaitambua kamati mpya iliyoteuliwa akibainisha kuwa madai ya kamati iliyovunjwa hayana mashiko. “Katiba yetu ipo wazi mamlaka ambazo zilikuteua kwa kutambua sababu basi inawajibika kuvunja na hupewi barua kwa sababu ni nafasi za kisiasa. Na kama wanaleta vurugu tunajua ni kundi la wahuni tunasubiria taarifa rasmi kwa viongozi tuwachukulie hatua,"amesema Ngulangwa.

Akizungumza na Mwananchi Digital baada ya vurugu hiyo katibu wa kamati iliyovunjwa, Suleiman Masahuni amesema wao bado ni viongozi halali,”tuna uhuru wa kuendelea kutumia ofisi hii na kueendelea kukijenga chama na tangu mwenyekiti kutoa tamko lake la kuvunja kamati Bbado hatujapewa barua rasmi ya kusitisha utendaji kazi wetu."

Masahuni amesema migogoro mingi inayoendelea ndani ya chama hicho inasababisha na viongozi wa kitaifa kwa kukumbatia makundi ya wachache badala ya kuangalia imani ya wananchama na uhai wa chama.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live