Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CUF Zanzibar kukagua ofisi zake

47898 Cufpic

Thu, 21 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Makamu mwenyekiti wa CUF Zanzibar,  Abass Juma Muhunzi amesema chama hicho kitafanya ziara katika ofisi zake zote Zanzibar baada ya kumalizika kile alichokiita ‘vurugu’ alizodai kufanywa na wanachama wa chama cha ACT-Wazalendo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Machi 21, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia vitendo vya ofisi za CUF kubadilishwa kuwa na ACT, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kujiunga na ACT.

Amesema licha ya kuwa na mpango wa kuyatembea matawi hayo ili kupanga mikakati kichama, lakini wakati huu hawawezi kufanya hivyo kutokana na wanachama wa ACT kupaka rangi za chama hicho ofisi za CUF.

"Kitendo cha kuyapaka rangi za ACT matawi yetu hakuna maana kwamba si ya kwetu. Bado  tunayatambua na muda ukifika wa kuyatembelea tutafanya hivyo"alisema .

“Tunafahamu watatutia hasara ya kuyabadili rangi matawi yetu, lakini haitajalisha kitu kwani tunajua wanachofanya bado hawakielewi.”

Soma Zaidi: Mikakati mipya ni muhimu CUF kukwepa njia iliyopitia NCCR-mageuzi



Chanzo: mwananchi.co.tz