Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA yatoa ratiba mapokezi ya Lissu kesho

Tundu Lissuww CHADEMA yatoa ratiba mapokezi ya Lissu kesho

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu anatarajia kupokelewa na maelfu ya wafuasi wa Chama hicho atakaporejea nchini kesho Januari 25, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Kamati Kuu ya mapokezi ya Lissu, Mch. Peter Msigwa, amesema Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya CHADEMA Uchaguzi Mkuu uliopita, atawasili nchini kesho jumatano saa Saba mchana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kwa Shirika la ndege la Ethiopia Airline.

Msigwa amesema Maandalizi yote ya mapokezi yameshakamilika, na Mara atakapowasili ataungana na viongozi wengine na wanachama wa Chama hicho kutoka uwanja wa ndege hadi uwanja wa Bulyaga Temeke mwisho utakapofanyika Mkutano wa hadhara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live