Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA yakataa kushiriki Uchaguzi Jimbo la Muhambwe

Chademapic 660x400.jpeg CHADEMA yakataa kushiriki Uchaguzi Jimbo la Muhambwe

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe lililopo Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.

Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa Mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika March 31, 2021 kwa njia ya mtandao wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na mazingira ya tume ya uchaguzi kutotenda haki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika May 2, 2021.

Chanzo: millardayo.com