Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA yajibu Mahojiano ya Rais Samia

MNYIKA 12 John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Mnyika, ametoa msimamo wa chama hicho kufuatia kauli ya Rais Samia aliyoitoa jana kwenye mahojiano aliyofanya jana na moja ya kituo cha habari cha Kimataifa, kuhusu mwenendo wa siasa, tozo za miamala, na kesi ya Mbowe.

Mnyika alimulika kwa ukubwa kuhusu kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, ambayo Rais Samia aliigusia hapo jana, kwa kusema kuwa ameingilia muhimili wa Mahakama hasa kwa kuwa shauri hilo tayari linasikilizwa Mahakamani.

"Nasema ni jambo kubwa, kwasababu Rais amezungumzia masuala yenye muelekeo wa kuingilia uhuru wa Mahakama na kuingilia mwenendo wa shauri ambalo tayari lipo Mahakamani, hili ni jambo kubwa katika nchi yenye misingi ya kidemokrasia ambayo inapaswa kuwa na mihimili isiyoingiliana , suala la Rais kuingilia jambo ambalo lipo na linaendelea mahakamani ni jambo kubwa, haliwezi kuachwa pasipokutolewa kauli na si tu kauli bali hatua zichukuliwe".

Aliongeza kusema kuwa hawataingia kwenye mtego wa kuzungumzia shauri ambalo tayari lipo Mahakamani, ila watatoa kauli baada ya tarehe 13 agust mwaka huu kuhusu kauli hii ya Rais.

Aidha aliongeza kusema kuwa kauli aliyoitoa Rais Samia kuhusu Mwenyekiti wa chama hicho kushitakiwa kwa makosa ya ugaidi tangu mwaka jana Septemba, si ya kweli kwakuwa hakuna kesi iliyofunguliwa mwaka jana mwezi huo kumuhusu mwenyekiti huyo.

"Kauli hii ya Rais ni ya uongo, ama rais amepotoshwa na watu wake, au rais ameamua kusema uongo, hakuna kesi yoyote ya ugaid au Uhujumu Uchumi ambayo mwenyekiti alifunguliwa mwezi septemba mwaka jana, kwa mara ya kwanza Mwenyekiti alifunguliwa kesi Mahakamani tareh 26 julai 2021, siku chache zilizopita, jamii ya Tanzania na kimataifa itambue kauli iliyotolewa na rais ni ya uongo".

Alitolea ufafanuzi kuhusu watu wengine ambao Rais Samia aliwataja kushitakiwa pamoja na mwenyekiti huyo kwa kesi ya Ugaidi na uhujumu uchumi, kuwa si ya kweli kwani watu hao walikamtwa Agosti 19 mwaka jana na sept 25 mwaka jana waliunganishwa na washtakiwa wengine watatu na kesi hiyo ilifutwa julai 27 mwaka huu.

Mnyika aligusia pia kuhusu kauli ya watuhumiwa wengine walioshtakiwa na mwenyekiti huyo kuwa wameshahukumiwa kuwa sio ya kweli kwani hakuna hukumu iliyotolewa na Mahakama yoyote kwenye kesi hiyo namba 61

"kesi ambayo bado taratibu zake hazijakamilika, inashangaza kusikia kutoka kwa Rais kuwa washtakiwa wengine wamesha hukumiwa, hii inaoonesha Rais anaingilia mahakama, anataka kutoa hukumu katika shauri amablo bado lipo Mahakamani"

Alileza kuwa tayari kama Chama wameshaelekeza wanasheria nini cha kufanya kufuatia kitendo cha Rais kuingilia Mahakama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live