Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA watoa tathimini mwaka mmoja wa Samia

Mbowe 1?fit=1080%2C720&ssl=1 Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuelekea kwenye kilele cha mwaka mmoja Rai Samia unaotimia Machi 19, 2022, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetoa msimamo wake kuhusu tathimini ya utendaji wake wa kazi kwa kusema kuwa kwa sasa wamejikita zaidi katika maendeleo ya chama chao.

Akitoa msimamo huo leo Machi 18, 2022 Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Aikael Mbowe amesema thathimini ya mwaka mmoja wa Rais Samia inafaa kutolewa na Katibu mwenezi wa CCM, Shaka Hamidu Shaka na sio CHADEMA.

"Mwaka mmoja wa Rais Samia utazungumzwa na Shaka, hilo swali la tathimini ya mwaka mmoja atalijibu Shaka mimi naomba niachieni ya CHADEMA" Amesema Mwenyekiti huyo.

Mbowe ameongeza kusema kuwa kwa sasa Chama hicho kimejikita katika kujijenga na kuwa hitaji kuu wanalolitaka ni kutolewa kwa kanuni za mikutano ya siasa ili vyama viweze kujijenga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live