Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA waomba kukutana na Rais Samia

MNYIKA123 John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia vuguvugu linaloendela hivi sasa nchini kuhusu mwenendo wa kisiasa hasa mara baada ya Rais Samia kuzungumza kuwa kuhusu utofauti wa siasa za kidemorasia na siasa za vurugu, chama cha Demokrasia na Maendelea CHADEMA kupitia Katibu Mkuu, John Mnyika kiumesema ipo haja ya kukiutana na Rais kuzungumza kuhusu mwenendo wa siasa

Mnyika ametoa kauli hiyo leo kwenye mkutano wa chama hiucho na waandishi wa habari jijini dar es salaam, alipokuwa akitolea ufafanuzi kuhusu mahojiano ya Rais Samia aliyoyafanya hapo jana, na kusema kuwa tayari walisha andika barua Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais

"Rais amesema yupo tayari kukutana na Vyama vya Siasa kwasababu Vyama vimejipanga, sisi tuliandika barua kwa Rais na tukaelezwa kuwa ameisoma mwenyewe na tutaelezwa tarehe ya kukutana, kimsingi ni vyema Ikulu ikaeleza kwanini mpaka sasa Rais hajakutana na CHADEMA"

Chadema imesema kuwa ipo haja kubwa ya kukutana na Rais Samia kwa mazungumzo kwani mambo yanaendelea kwa sasa sio rafika kwa ustawi wa siasa nchini.

“Tulipanga kukutana na Rais juu ya mambo yaliyotokea katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ila pia yamejitokeza mengine ambayo kuna haja ya haraka ya kuzungumza na Rais, hatujafunga milango ya mazungumzo na Rais, tunasubiri Ikulu itupe tarehe”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live