Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA wajibu kauli ya Jaji Mutungi kwa kuwataka Polisi kufuata Sheria

Chadema23 Tamko CHADEMA, wataka Jeshi la Polisi lifuate taratibu

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema kimesema kitafuata sheria kwa mujibu wa katiba na kuvitaka vyombo vingine na mamlaka kufuata sheria pia.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, na kuongeza kuwa wao kama chama wataedelea na shughuli zao za kichama ikiwa ni pamojana kuendesha vikao vyao na kulitaka jeshi la Polisi kufuata sheria kama katiba inavyoeleza.

“Sisi Chadema tutaendelea na mikutano na vikao mbalimbali kwa mujibu wa sheria, Polisi wafuate sheria, Msajili afuate sheria, sisi Chadema tufuate sheria na CCM ifuate sheria kama Katiba inavyoelekeza,” amesema Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema.

Katika mkutano huo, Mrema amesema kuwa kama kila mmoja akitii sheria watakuwa kwenye mstari mmoja na hakutakuwa na haja ya vyama na polisi kupatanishwa kwani kila mmoja atajua mipaka ya kazi yake.

Tamko hili linakuja siku moja baada ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi kuadhimia kukutana na Vyama vya siasa pamoja na Jeshi la Polisi nchini kwa ajili ya mazungumzo ili kufikia muafaka kwa pande zote mbili.

Aidha Chadema imetoa wito kwa Msajili, kwa kumuandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi, ya kumuonya aache kuvunja Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuingilia shughuli halali za vyama vya siasa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live