Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA wajibu hoja, Serikali ikiwaunga mkono kina Mdee

Mdee Mak.jpeg CHADEMA wajibu hoja, Serikali ikiwaunga mkono kina Mdee

Thu, 30 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mawakili wa Halima Mdee na wenzake 18 kumaliza kuwasilisha hoja za kuomba ridhaa ya kufungua kesi kupinga wabunge hao kuvuliwa uanachama wa Chadema, mawakili wa chama hicho nao wamezijibu hoja hizo.

Leo Alhamisi Juni 30, 2020 mchana Jaji Mustapha Ismail katika Mahakama Kuu Masjala Kuu Dar es Salaam alianza kusikiliza sababu za Halima Mdee na wenzake 18 kuomba ridhaa ya kufungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Akijibu hoja hizo, kiongozi wa jopo la mawakili wa Chadema, Peter Kibatala japo alikubali kuwa kina Mdee wana maslahi na haki ya kuja mahakamani, lakini alipinga kuwa maombi yao yamefunguljwa nje ya muda.

Kibatala alidai kuwa kikomo cha muda kinahesabiwa kuanzia uamuzi wa awali wa Kamati Kuu ukiotolewa Novemba 27, 2020.

Katika kuunga mkono hoja yake hiyo, Kibatala aliwasilisha mahakamani uamuzi wa kesi mbalimbali zilizowahi kuamuriwa na Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na mahahakama za nje, ikiwemo Mahakama ya India.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live