Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA waitaka Serikali ifute kesi ya Mbowe

Mbowe Pc Data Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, John Mnyika ameitaka Serikali kuiondoa kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwani ina chafua sifa ya Mahakama kimataifa.

Ametoa kauli hiyo Oktoba 21, 2021 wakati wa mkutano wa viongozi wa chama hicho na waandishi wa habari na kuongeza kuwa Mwenyekiti huyo amebambikiziwa kesi ya ugaidi mara tu baada ya kuanzisha harakati za kudai Katiba mpya.

"Serikali ili isiendelee kuiharibu Mahakama kwasababu ya kesi ya Mbowe, Serikali iiondoe hii kesi Mahakamani kwasababu kesi ilikuwa ya kisiasa hadi Mbowe akabambikiziwa kesi ya ugaidi ikiwemo madai ya Katiba mpya na Tume huru yaachwe yashughulikiwe kisiasa, jinai haiwezi kuminya kilichoitwa chokochoko ya Katiba Mpya"

"Natoa rai kwa Mahakama bila kuingilia uhuru wa Mahakama, Viongozi wa Mahakama wakumbuke pamoja na udhaifu wa katiba lakini ibara ya 107 a (1) inasema Mamlaka yenye kauli ya mwisho kutoa haki Katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama, kwahiyo kauli ya haki ya Mbowe haiwezi kuwa ni kauli ya Rais, IGP wala yoyote, wenye haki na Mamlaka ni Mahakama, kama Serikali haitofuita kesi hii Mahakama itambue ukuu wake wa haki" Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live