Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA kuchaguana Kanda ya Pwani, Sumaye kupigiwa kura ya ndio au hapana

86248 Pic+chadema CHADEMA kuchaguana Kanda ya Pwani, Sumaye kupigiwa kura ya ndio au hapana

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Kanda ya Pwani inafanya uchaguzi wake leo Alhamisi Novemba 28, 2019 kupata viongozi watakaoongoza kanda hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumza na Mwananchi na Mwananchi, Ofisa Oganaizesheni na Uchaguzi Kanda hiyo yenye mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, Christopher Mbusule amesema uchaguzi huo unafanyika katika ukumbi wa Njueni uliopo Kibaha Mjini mkoani Pwani.

Amesema tayari kamati kuu imepitisha na kurudisha majina ya wagombea ambapo nafasi ya mwenyekiti anayetetea nafasi yake ni Frederick Sumaye, waziri mkuu mstaafu ambaye ni mgombea pekee.

"Kamati kuu imeshapitisha majina ya wagombea kwa nafasi ya mwenyekiti Sumaye ambaye anatetea nafasi yake utaratibu wa kura za za ndio au hapana utatumika kwa kuwa mgombea yuko yake," amesema Mbusule

Awali, kabla ya kamati kuu nafasi ya mwenyekiti walikuwa wagombea wawili ambao ni Frederick Sumaye na James Haule ambalo jina lake halikurudi.

Katikanafasiyamakamumwenyekiti,                                                                                                                                           Mbusule amesema majina yaliyopitishwa ni manne ambayo ni  Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani, Baraka Mwago watachuana kwenye hiyo nafasi.

Ruth Mollel na Diwani Majohe Waziri Mwenevyale.

Katika nafasi ya mweka hazina majina yaliyopitishwa ni Florence Kasilima, Joseph Zahabu, Michael Mtally na Omar Mkama.

Uchaguzi huo ni mwendelezo wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa ndani kwa ngazi ya mabaraza ya wazee, vijana na wanawake na kuhitimishwa na uchaguzi wa viongozi wa kitaifa utakaofanyika Desemba 18, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz