Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA Yajibu Hoja Samia kuhusu Siasa za "Demokrasia/Fujo"

MNYIKA WEB John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kimepinga kauli ya Rais Samia aliyoitoa kuhusu utofautii wa Demokrasia ya Kisiasa na siasa za vurugu, kwani kauli hiyo inapingana na Katiba na Sheria ya vyama vya siasa hasa katika kifungu cha 11 ambacho kinaeleza kuhusu haki za kisiasa.

Akizungumza kwa niaba ya Chama, John Mnyika ambaye ni Katibu Mkuu, amedai kuwa kauli hiyo haipo kikatiba kwani inaminya uhuru wa Vyama vya Siasa, kwani Sheria ya vyama ina eleza bayana kuwa imeruhusu vyama kufanya siasa za hadhara ili kujipatia wanachama wapya, hivyo wanaiona kauli hiyo kama mbinu ya kudhibiti vyama vya siasa.

"Rais ametumia mfano wa Marekani, kuwa uchaguzi ukiisha vyama vya siasa vinakaa kimya vina tulia, Marekani anayoizungumza Rais ,Samia wakati wa utawala wa Trump ilikuwa na mikutano ya kisiasa na hata maandamano kama Black Lives Matters, hivyo kauli hii si ya kweli."

Wamedai kuwa maelezo hayo ya Rais Samia si ya kweli, huku wakimulika kwa mfano kuhusu Operation walioifanya nchi nzima iliyoitwa Operation Haki kuwa ilimalizika amani pasipo kuvunja sheria wa la kufanya uharibu wowote

Chanzo: www.tanzaniaweb.live