Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA YAAHIDI KUREJESHA ZAO LA PAMBA TABORA

YUDF87IH.webp CHADEMA YAAHIDI KUREJESHA ZAO LA PAMBA TABORA

Mon, 21 Sep 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amesema iwapo chama hicho kitapata ushindi kitahakikisha watu wa mkoa wa Tabora wanarudishiwa kilimo cha zao la pamba na kuhakikishiwa upatikanaji wa soko la zao hilo.

Hayo ameyasema jana Septemba 20, 2020, wakati akinadi sera za chama hicho katika mkoa huo na kusema chama hicho ndio chenye Ilani bora ambapo amewaomba wananchi kukichagua chama hicho ili waweze kuleta mageuzi ya kiutawala.

“Watu wa Tabora Kaskazini mkituchagua tutahakikisha tunawarudishia zao lenu la pamba na tutahakikisha pamba yenu mtaweza kuuza sehemu kwa yeyote mnayemtaka sio kwenye vyama vya ushirika vinavyowakopa pamba yenu,’’ alisema Salum Mwalimu

“Hiki ni kipindi cha kupanga upatikanaji wa elimu bora, upatikanaji wa maji safi, soko la tumbaku yetu na upatikanaji wa soko la pamba yetu,’’.

Chanzo: zanzibar24.co.tz