Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA, Wafanya Maombi maalum kwa Mbowe

MAOMBI Wanachama wakifanya Maombi

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, leo walikusanyika katika ofisi za chama hicho na kufanya maombi maalum ya kumuombea mwenyekiti wa chama hicho Freema Mbowe, maombi yaliyoendeshwa na Amosi Hulilo ambaye ni Askofu wa kanisa la Evangelical Pentecostal Restoration Church (ERPC)

Akizungumza kabla ya maombi hayo, Askofu Hulilo amewataka wanachama hao kutokata tamma katika mapambano yenye kuleta ukombozi wa taifa kwa ujumla

"Kama nia yenu ni njema basi Mungu ataibariki, lakini kama siyo njema basi hataibariki, hivyo kama mnadhamiria kufanya ukombozi, haki na amani aminini kuwa magumu mnayopitia ndiyo mnakaribia kupata ukombozi huo," .

Pia, Askofu huyo alitumia fursa hiyo kumuombea Rais Sama apate washauri watakao muongoza vyema pia mungu ampe afya nje aongeze taifa kwa haki

Hata hivyo wakati maombi yakiendelea, magari ya polisi zaidi ya manne yakiwa na askari waliojihamia kwa kubeba silaha walikuwa wakifanya doria umbali wa takribani mita 100 kisha wakaondoka wakati maombi yakiendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live