Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CHADEMA: Hatutaingilia Mahakama sakata la kina Mdee

Mdee Mak.jpeg Wabunge 19 waliovuliwa uanachama CHADEMA

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema Chama hicho hakitaingilia taratibu zinazoendelea Mahakamani kuhusu Wabunge 19 waliofutiwa uanachama

Amesisitiza kuwa, Kamati Kuu haikuwahi kuteua Wabunge wa Viti Maalum na CHADEMA haitambui Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 wala hawatashiriki wala kupokea matunda yoyote ya matokeo ya uchaguzi huo

Amesema hawatambui Jimbo moja ambalo CHADEMA ilitangazwa kushinda, Wabunge wa Viti Maalum 19 wala Ruzuku ya Tsh. Milioni 107 ambayo ilitangazwa kwamba CHADEMA ilistahili. Pia ametoa wito wa kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu chini ya Tume Huru ya Uchaguzi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live