Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yazingatia maono ya JPM, Mwinyi

De8cdbf695254e606f72fc5bd9630978 CCM yazingatia maono ya JPM, Mwinyi

Wed, 2 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, kimeteua wagombea ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar kwa kuzingatia maono ya chama hicho, ya mgombea urais visiwani humo Dk Hussein Mwinyi na ya mgombea urais wa Tanzania John Magufuli.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema uteuzi huo pia umezingatia uwakilishi wa kimakundi rika, mazingira ya Zanzibar, maisha ya leo na kuangalia watu wanaoweza kuleta mawazo mazuri kuhakikisha Zanzibar inapata wawakilishi wanaosadifu maono hayo.

Polepole aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, Kamati Kuu (CC) chini ya Rais John Magufuli iliyokutana jijini humo imejadili, imetafakiri, imezingatia uhodari na ubingwa wa wagombea hao.

Alisema, wagombea hao wamechaguliwa kuwania nafasi za uwakilishi kutokana na uwezo wao wa kuchangia katika kuleta maendeleo ya Zanzibar pamoja na mustakabali wa sasa na baadaye kwamba utakuwa katika mikono salama.

"Tumeshajipambanua kwamba suala la maendeleo kule Zanzibar si mjadala, mwendokasi wa watu wa Zanzibar halina mjadala, tumefanya utafiti mkubwa na kujiridhisha Wazanzibar wanataka ule muziki wa Magufuli wa Muungano pia uakisiwe Zanzibar."alisema na kuongoza;

"Tumepata mtu mpole, mnyenyekevu wa hali ya juu, amehudumu kama kiongozi mwandamizi katika serikali ya Muungano na Zanzibar," alisema DK Mwinyi anaweza kuwavusha na kuwafikisha mapema zaidi.

“Hiyo ndiyo ya timu ya ushindi Zanzibar ambayo ilianza tangu kwenye kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kwa kuteua wabunge na lengo tumekamilisha safu ya ushindi katika serikali ya Jamhuri JPM baada ya kuzindua Kampeni Agosti 27, mwaka huu jijini Dodoma” alisema Polepole na kusema CCM ina uhakika wa kuleta maendeleo ya haraka Zanzibar.

"Baraza la Wawakilishi ni chombo cha uhakika mno tulihakikisha kwenye Ilani 2020-2025 ambayo ni kubwa mara tatu ambayo inajua wananchi makini wanaotambua changamoto za Zanzibar."

Alisema kwa kuzingatia ratiba ya Zanzibar wagombea wa CCM kisiwani huko watatakiwa kuhakikisha masharti ya ratiba ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), na wanazingatia kanuni na kufuata sheria.

Polepole alisema chama hicho kimeshaandaa mawakili 76 kuhakikisha kwamba hakuna mapingamizi ili kutoa ushauri elekezi wa namna ya kushiriki uchaguzi.

“Wasitegemee hoja ya mapingamizi tumewekeza vya kutosha amani, mshikamo, na upendo utulivu…ndugu yetu Dk Hussein Mwinyi anapanga mambo kwenda kwa mwendo kasi ya Magufuli. Katika kufanya hivyo inatakiwa wawakilishi makini wanaoweza kulinda maslahi ya Zanzibar”alisema.

Aliwataja walioteuliwa kugombea kuwa ni Zawadi Amour Nassoro katika jimbo la Konde, Shenata Shaane Khamis (Micheweni), Said Saleh Salim (Tumbe),Tumu Mwalim Masoud (Wingwi), Mariam Dhai Juma (Gando), Makame Said Juma (Kojani), Othman Ali Khamis (Mtambwe), Khamis Dadi Khamis (Pandani), Harous Said Suleiman (Wete), Nadir Abdulatif Yusuph (Chanani) na Juma Makungu Juma (Kijini).

Wengine ni Abdallah Abbas Wadi (Nungwi), Sulubu Kidongo Amour (Mkwajuni),Haji Omar Kheri (Tumbatu),Mtumwa Bee Yusuph (Bumbwini),Ali Salum Mohamed (Donge), Asha Abdallah Mussa (Mahonda), Shaibu Hassan Kadiara (Chakechake), Suleiman Masoud Makame (Chonga) na Masoud Ali Mohamed (Ole).

Wengine ni Bakari Ahmad Bakari (Wawi), Suleiman Makame Ally (Ziwani), Bahati Khamis Kombo (Chambani), Mussa Foum Mussa (Kiwani), Abdallah Hussein Kombo (Mkoani), Mohamed Mganza Jecha (Mkoani), Issa Haji Ussi (Chwaka), Simai Mohamed Said (Tunguu),Haji Shaaban Waziri (Uzini), Haroun Ali Suleiman (Makunduchi), Dr Sudi Dou Hassan (Paje) na Mwanaasha Hamis Juma (Dimani).

Wagombea wengine ni Yusuph Hassan Idd (Fuoni), Suleiman Khamis Suleiman (KiembeSamaki), Ameir Abdallah Ameir (Mwanakwerekwe), Ally Suleiman Ameir (Pangawe),

Wagombea kupitia Viti Maalumu ni Shadiz Mohamed Suleimani , Zuhura Mgeni Othumani na Zainabu Omari Amiri ( Mkoa Kusini Pemba), Salma Mussa Bilal, Rahma Kassim Ally na Arafa Ally Yusufu (Mkoa Kusini Unguja), Fatima Ramadhani Mandoba, Mwanaidi Kassim Mussa na Fatma Ally Ameir ( Mkoa Magharibi).

Wengine ni Mudrick Ramadhani Soradi (Bububu), Machano Othuman Said (Mfenesini), Hussein Ibrahim Makungu (Mtoni), Mihayo Juma Mhunga (Mwele), Hassan Hamis Hafidhi (Welezo), Rukia Omari Mapuli (Amani), Miraj Khamis Mussa (Chumbuni), Jamal Kassim Ali (Magomeni), Shabani Ali Othuman (Mpendae), Hamuza Hassan Juma (Shauri Moyo), Ali Abdulgulam Hussein (Jang'ombe), Nasoro Salum Ali (Kikwajuni), Yahaya Rashid Abdullah (Kwahani) na Muhammed Ahmada Salum (Malindi)

Wagombea wengine ni Saada Ramadhani Mwendwa, Mgeni Hassan Juma na Salma Abdi Ibade (Mkoa Mjini), Mwantatu Mbaraka Hamisi na Zainab Abdallah Salum (Wenye Ulemavu), Riziki Pembe Juma( Wasomi), Salha Mohamed Mwinjuma na Udhaima Mbaraka Tahir (Wawakilishi wa Vijana), Sabiha Filifili Tani (Wazazi).

Chanzo: habarileo.co.tz