Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yazindua barabara Kibaha Pwani

Swampa Viongozi toka vyama tofauti vya ukombozi barani Afrika wakizindua barabara hiyo

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amefungua barabara ya Ukombozi ya Kilomota 1.8 inayokwenda Chuo Cha Uongozi Cha Siasa Cha Mwalimu Nyerere kilichopo eneo la Chang'ombe Kata ya Kwamfipa Halmashauri ya Kibaha Mjini Mkoani Pwani.

Akifungua barabara hiyo leo Chongolo amewataka wananchi wa eneo hilo la Kwamfipa kulinda miundombinu ya barabara hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kujiimarisha kiuchumi.

"Ukombozi tunaoenda nao baada ya kufungua barabara hii ni pamoja na kujikomboa kiuchumi hivyo wito wangu kwenu wana Pwani lazima na ninyi mtengeneze programu za kujiendeleza pia muweke mifumo mizuri na yenye tija na kutumia ufunguzi wa barabara hii kwa kuwa ni muhimu sana kwenu hivyo mnao wajibu wa kuitunza " alisema Komredi Chongolo.

"Nimeona mmeanza kutupa takataka pembezoni mwa barabara hili jambo nalikemea kwa sauti kuu kwamba siyo sahihi hivyo ngazi zote za uongozi msimamie usafi wa barabara hii pamoja na kuitunza" alisema Chongolo,

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha Erasto Mpangala alisema kuwa awali eneo hilo lilikuwa katka hali mbaya sana na haikuwa rahisi kupitika hivyo ujenzi wa barabara hiyo inayokwenda Chuo Cha Mwalimu Nyerere huku aliongeza kwa kusema kuwa kwa sasa milango imefunguka kwa wakazi wa eneo hilo kwa kuwa na muingiliano kiuchumi umekua hivyo jamii husika inapaswa kuilinda.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Selina Wison ameishukuru serikali ya watu wa China pamoja na vyama rafiki vya ukombozi Kusini mwabara la Afrika kwa ujenzi wa barabara hiyo huku akiahidi kushirikiana na wananchi kutunza miundombimbinu ya barabara hiyo.

Mbunge Mstaafu wa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zainab Vulllu alisema kua wakaazi wa Pwani tunamshukuru Mungu tunasema huu ni ukombozi mkubwa sana hasa kwa kina mama kwani wao ndiyo wanufaika zaidi kwa sababu ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha familia nzima kwa ujumla,

Wengine walioshuhudia ufunguzi wa barabara hiyo ni pamoja na wawakilishi wa makatibu wenza kutoka katika nchi zilizopo Kusini mwa Afrika ambao ni Sofia Chinengwa kutoka Chama Cha (SWAPO) Namibia, Manueli Domingo Agusto kutoka (MPLA), Fransisco Mkatlea (FRELIMO) Msumbiji,Sibongile Dasani( ANC) Afrika Kusini.

Chuo hicho ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa vyama vitano ambavyo vilikua katika mstari wa mbele wa kupigania uhuru Kusini mwa Afrika kitazinduliwa kesho (Jumatano) na Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live