Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yaweka wazi siku ya kumtangaza mgombea Urais

94867 Pic+polepole CCM yaweka wazi siku ya kumtangaza mgombea Urais

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, ametoa ratiba ya mchakato wa kuteua wagombea ndani ya Chama hicho kwaajili ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2020.

Akiongea leo Juni 12, 2020 mbele ya waandishi wa habari amesema, watakaoomba nafasi za kugombea wanatakiwa kujua maono ya kiongozi wa chama, Dkt John Magufuli ili wakamsaidie katika kutekeleza majukumu yake huku wakijua wazi kuwa rushwa ni adui wa haki.

''Wagombea wetu tunataka wawe wapole, wanyenyekevu na wenye nidhamu sana ili Chama kikija kuamua kumpitisha basi awe ana sifa zote za kusimama kuiwakilisha CCM'', amesema.

''Julai 6 - 7 kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM itakaa kwaajili ya kuanza uchuchaji wa wagombe. Julai 8 ni kikao cha kamati ya usalama na maadili na kisha Julai 9 ni Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu kwaajili ya mapendekezo ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea'', amesema.

Aidha amefafanua kuwa, ''Julai 11 na 12 utaketi Mkutano Mkuu wa CCM taifa ambao utakuwa na kazi ya kuchagua jina moja la mwanachama ambaye atasimama kuiwakilisha CCM katika majina matatu yatakayokuwa yamepitishwa na Kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya taifa''.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live