Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yawataka viongozi wake kueleza mafanikio ya Serikali

A83c8eec2dd04e145099b3b8f9591011 CCM yawataka viongozi wake kueleza mafanikio ya Serikali

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), wametakiwa kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanayotokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawale wa chama hicho (UWT), Gaudentia Kabaka, wakati akifungua kongamano la kumuombea na kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM nchini lililofanyika Juni 11, 2022, Uwanja wa Jamhuri, Moropgoro.

Kabaka alisema ni jukumu la viongozi wote wanatokana na CCM kujitokeza mstari wa mbele kuyasemea maendeleo yote yaliyoletwa na serikali, ikiwemo ya Awamu ya Sita, ili wananchi wayajue badala ya kusubiri kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2025.

“ Kwa hiyo niwaombeni viongozi wote tumsaidie Mama Samia ambaye ni Rais wetu. Kuna madiwani wetu, tuna wabunge wetu tumsemee mama Samia katika maeneo yenu kwenye kata zenu na majimbo yenu miradi hii ipo huko.

“Nyie viongozi ndiyo wa kumsemea kwa uhakika kwa wananchi, ili ikifika 2025 iwe tu ni kuwakumbusha wananchi na sio kuanza kuwaambia tumefanya hiki wao wawe tayari wanajua, “ alisema Kabaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live