Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yawataka Madiwani, watumishi kuacha 'kuwindana'

Ccm Pic Data CCM yawataka Madiwani, watumishi kuacha 'kuwindana'

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini kimewataka madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kufanya kazi kwa kushirikiana kama timu na kuacha kuwindana.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Moshi mjini, Alhaji Omari Shamba wakati kamati ya siasa ilipotembelea na kukagua ujenzi wa madarasa 22 ya shule za sekondari, yanayojengwa kwa fedha za Uviko-19.

Alhaji Shamba amesema ili kazi za madiwani ziweze kuwa nyepesi na nzuri, ni lazima wafanye kazi kwa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa idara pamoja na watumishi wote wa halmashauri na si kutafuta uadui au kuwindana.

"Kazi kubwa ya chama ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma na huduma hizi zinafanywa na watumishi na watendaji wa halmashauri, hivyo hatuwezi kuwa maadui, niwaombe madiwani mtambue ili kazi iwe nyepesi na mfanye kazi nzuri ni lazima mshirikiane na kuheshimiana na wakuu wa idara na watumishi wote wa halmashauri"

Ameongeza kuwa "Kama ni kuwawakemea wawakemee na wawakosoe pia, lakini si kwa uadui, iwe ni kwa ajili ya kujenga, na wasikae kuwindana, kati ya madiwani na watumishi, washirikiane kwa karibu na kufanya kazi kama timu moja, ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa kikamilifu"

Katibu wa CCM Moshi Mjini, Ibrahim Mjanakheri ameutaka uongozi wa Manispaa hiyo kuhakikisha miradi yote inayopaswa kutekelezwa katika Manispaa hiyo inatekelezwa kwa kasi kama ilivyofanyika kwenye miradi ya Uviko-19.

Advertisement Mhandis wa Manispaa ya Moshi, Richard Sanga amesema walipokea Sh440 milioni, kutoka mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19, kwa ajili ya kujenga madarasa 22, katika shule za sekondari 10.

"Mpaka sasa tupo asilimia 95 ya ukamilishaji wa madarasa hayo, na tumejiwekea mkakati ifikapo Desemba 10, tuwe tumekamilisha ujenzi wa madarasa ikiwa ni pamoja na kuweka viti na meza na hivyo ifikapo Desema 15 Manispaa ya Moshi tutakuwa tumekamilisha ujenzi wa madarasa haya, kama maagizo ya Rais yalivyotaka"

Ofisa elimu Sekondari katika Manispaa hiyo, Agnes Luhwavi, amesema madarasa 22 yanayojengwa kwa mpango wa Covid-19, yanakidhi upungufu uliokuwepo na wanafunzi wote 3,371 wa kidato cha kwanza ambao watapokelewa januari 2022, wataingia madarasani pindi shule zitakapofunguliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live