Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yawaonya watendaji wa Serikali wanaoshabikia upinzani

12575 CCM+PIC TanzaniaWeb

Sat, 18 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Arusha kimewataka watendaji wa Serikali mkoani humo wenye mapenzi na vyama vya upinzani kwa kipindi hiki wanapaswa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama hicho tawala.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Agosti 18, 2018 na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Loota Sanare wakati akizungumza na  wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwsa).

Ilikuwa ni katika hafla ya kutia saini mradi wa kuboresha mfumo wa maji taka  katika jiji la Arusha unaogharimu Sh77.2bilioni.

Amesema kwa sasa Serikali ya CCM ipo madarakani ni lazima watendaji wa Serikali kutekeleza ilani.

“Tunajua kuna baadhi ya wafanyakazi wa Serikali ni wapenzi wa vyama vya upinzani lakini lazima mtuvumilie, subiri vyama vyenu vije kutawala lakini sasa tunatekeleza Ilani ya CCM pekee,” amesema.

Amesema katika kuhakikisha Ilani inatekelezwa, viongozi wa CCM watakuwa wakipita kuangalia miradi yote inayofadhiliwa na Serikali na kuona kama inafanya kazi vizuri kwani wao ndio watabanwa na wananchi wakati wa uchaguzi.

“Tutapita kwenye miradi kuona kama inatekelezwa vizuri, kama tukipata malalamiko, sisi tutamwambia mwenyekiti wetu, Rais John Magufuli kuwa kuna watendaji hawatekelezi vyema Ilani hivyo hawafai waondoke,” amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz