Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yatuma salamu za Idd elFitr ikisisitiza umoja na amani

7feeb960330db4efc8245d5326181cb1.jpeg CCM yatuma salamu za Idd elFitr ikisisitiza umoja na amani

Sun, 16 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetoa salamu za Sikukuu ya Idd el-Fitr na kutaka Watanzania wa dini zote nchini kuendelea kudumisha amani, umoja, utulivu na mshikamano katika taifa .

Vile vile kimeomba kupitia sikukuu hiyo Watanzania waendelee kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili Mungu amjalie afya njema, maono na msimamo dhabiti na kuendelea kusimamia amani, utulivu na usalama.

Katika salamu hizo za chama zilizotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka (pichani) alisema Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa nchi Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wanachama, watendaji na viongozi wa CCM wanatoa salamu za heri ya Sikukuu ya Idd elFitr kwa waumini wa dini ya kiislamu.

“Uongozi wa chama unaendelea kutoa wito kwa Watanzania wa dini zote kuendelea kuiombea nchi na kumuunga mkono mwenyekiti wetu katika hatua mbalimbali anazochukua kwa maslahi mapana ya taifa na kuboresha uchumi na maisha ya Watanzania wote,”alisema.

Pia chama kimewataka Watanzania wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ,ubunifu na maarifa ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla huku wakihimiza serikali zake mbili kuweka mzingira wezeshi ya ajira na kujiajiri.

Wakati huo huo, Shaka jana alishiriki swala ya Idd el-Fitr Mkoa wa Kigoma iliyoswaliwa katika Uwanja wa Stendi Mpya ya UjijiKigoma.

Swala hiyo iliyoongozwa na Shehe wa Mkoa wa Kigoma, Shehe Hassan Kiburwa ilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Juma Duni Hajji, Waziri wa

Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Suleiman Jafo, Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Kilumbe Shaban Ng’enda, Mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hillary na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Maryam Ditopile.

Chanzo: www.habarileo.co.tz