Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yatuma salamu kwa wapinzani, 'wembe ni ule ule'

Ef9c2c6424e064b4dbfa358ea92b4bab CCM yatuma salamu kwa wapinzani, 'wembe ni ule ule'

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuph Makamba, amevitaka vyama vya upinzani nchini, vijitayarishe kuchuana na Rais Samia Suluhu Hassan, katika kinyang’anyiro cha urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwani wembe ni ule ule.

Makamba ametoa kauli hiyo leo Aprili Mosi, 2022, jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.

“Mama nilikusikia ukiongea na wanawake ukawambia hawakuchagua Rais mwanamke, Rais mwanamke watamchagua 2025…huyu mwanamke ni nani, nikamuliza mama Januari ni wewe akasema ahaaaa Mungu aninusuru, nikampigia Kate Kamba (Mwenyekiti CCM Mkoa) nikamuliza ni wewe akasema akuuu… nikampigia simu Jenista Muhagama maana yeye anajiita mama Februari nikamuliza ni wewe…akasema haa Mungu aninusuru. Huyu mwanamke ni wewe, nawaambia viongozi wa upinzani mpo hapa, 2025 mgombea ni yule, kama kuna anayejiandaa huko akae tayari,” amesema Mzee Makamba.

Katibu Mkuu mstaafu huyo wa CCM, amesema katika kipindi cha uongozi wake akiwa Makamu wa Rais na sasa Rais wa Tanzania, Samia amefanya mambo mengi mazuri.

“Sisi Simba tuna kocha mzuri hawezi leo mtu akatuambia badilisheni kocha, hatutaki, Yanga wana kocha mzuri hata Simba anaogopa huu ubingwa nitaupata? Sasa Mama Samia alikuwa kocha msaidizi chini ya Magufuli, Mungu akamchukua tukamfanya kocha magoli yanaingia. 2025 mnaenda na nani tena?” amehoji Mzee Makamba.

Aidha Makamba amesema Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), imefanya jambo sahihi kumteua Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa atamsaidia Rais Samia kushinda kwenye uchaguzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live